JAMII YASHAURIWA KULINDA TAARIFA BINAFSI
Oct. 24, 2024, 4:08 p.m.Katika hatua ya kuhakikisha Ulinzi wa faragha za wananchi unazingatiwa kwa mujibu wa Sheria nchini, Jamii yashauriwa kulinda taarifa zao kwa kutokuzitoa kwa Taasisi ambazo hazijasajiliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa binafsi (PDPC).
Wito huo umetolewa jijini DSM na Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji – PDPC, Mhandisi Stephen Wangwe wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Crown FM kupitia kipindi cha Kasri la Kikeke ambapo amesema kwasasa PDPC wanasajili na kutoa vyeti kwa Taasisi zote zinazochakata na kukusanya Taarifa nchini hivyo kabla hujatoa taarifa zako hakikisha kama wamesajiliwa.
“Kabla ya kutoa Taarifa zako kwa Taasisi yoyote nchini hakikisha kama wamesajiliwa na kupata cheti cha PDPC, hii itawezesha PDPC kusimamia ulinzi wa Taarifa za watu na faragha zao.” amesema Mhandisi Wangwe
Aidha Mhandisi Wangwe amesema PDPC wanatarajia kuandaa kanzi data (Database) ambayo itaonesha ni Taasisi zipi zimesajiliwa na kupata vyeti ili wananchi wawe huru kutoa taarifa zao pale zinapohitajika.
Katika hatua nyingine Mhandisi Wangwe akatoa wito kwa Wadau wa Maendeleo hasa vyombo vya habari kushirikiana na PDPC kutoa elimu katika jamii kuhusu dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
“Sisi kama Tume tunashirikiana na wadau mbalimbali na hapa pia nitoe wito kwa hizi media groups na wengine wote wanaofanya kazi za uelimishaji kuja kwetu kuona namna gani tutashirikiana kuona tunafikisha hii elimu kwa jamii, husasani vyombo vya habari vya kijamii (Community Media)”. Amesema Mhandisi Wangwe
PDPC AND TIRA TO BUILD SUSTAINABLE…
IN DIGITAL ECONOMY PRIVACY SHOULD …
CONTACT US
Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Masha…
ULINZI WA TAARIFA BINAFSI UNAANZA …
JAMII YASHAURIWA KULINDA TAARIFA B…
PDPC KUSHIRIKIANA NA WADAU KUIMARI…
PDPC NA HILTON LAW GROUP WAKUTANA …
TUZINGATIE KANUNI ZA DHANA YA ULIN…