ULINZI WA TAARIFA BINAFSI UNAANZA NA WEWE MWENYEWE
Oct. 23, 2024, 10:58 a.m.Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) - Bw. Innocent Mungy ameitaka jamii kuielewa dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi na kuhakikisha wanalinda taarifa zao kwa kuzitoa pale tu zinapohitajika.
Bw. Mungy amesema hayo akiwa kwenye mahojiano maalum TBC katika kipindi cha Jambo Tanzania ikiwa ni muendelezo wa utoaji wa elimu kwa umma kuhusu uwepo na utendaji kazi wa PDPC.
“Dhana ya mifumo kusomana ipo kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa urahisi na haki ya mhusika wa taarifa ya kutoa ridhaa pale taarifa zake zinapotumika na mifumo ya watoa huduma. Huu ni mpango mahsusi wa kulinda faragha za wananchi.”
Bw. Mungy ameongeza kwamba, kupitia muundombinu wa Taifa wa kubadilishana taarifa kati ya Taasisi za umma na binafsi ujulikanao kama Jamii X-Change, PDPC imeweka mazingira yatakayo muwezesha mhusika wa taarifa kujua taarifa zake zimetumika wapi, wakati gani na zimetumikaje na hivyo kuwa na haki ya kutoa malalamiko iwapo zimetumika bila ridhaa yake.
Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi imeweka misingi nane ya ulinzi wa taarifa binafsi, misingi hiyo inatakiwa kuzingatiwa na wakusanyaji na wachakataji wa taarifa kwa ajili ya huduma mbalimbali ili kulinda utu na faragha ya muhusika wa taarifa.
Moja ya msingi hiyo ni kuhakikisha kwamba taarifa hizo zinakusanywa kwa ridhaa ya mhusika wa taarifa, zinalindwa na zisitumike kinyume na makubaliano baina yake na mtoa huduma.
PDPC inasimamia na kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa kwa ufasaha ili kulinda faragha za watu na inapenda kuzikumbusha Taasisi zote za umma na binafsi zinazokusanya na kuchakata taarifa ambazo bado hazijatambuliwa na PDPC, kujisajili na kupata cheti kama hatua ya awali ya kuitambua na kuitekeleza sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
PDPC AND TIRA TO BUILD SUSTAINABLE…
IN DIGITAL ECONOMY PRIVACY SHOULD …
CONTACT US
Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Masha…
ULINZI WA TAARIFA BINAFSI UNAANZA …
JAMII YASHAURIWA KULINDA TAARIFA B…
PDPC KUSHIRIKIANA NA WADAU KUIMARI…
PDPC NA HILTON LAW GROUP WAKUTANA …
TUZINGATIE KANUNI ZA DHANA YA ULIN…