JAMII X-CHANGE; UBUNIFU KATIKA MIFUMO KUSOMANA
Aug. 19, 2024, noonBaadhi ya viongozi kutoka Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar) wakifuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa maelekezo ya Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ya kutaka Mifumo yote ya Serikali na Binafsi isomane ifikapo Disemba 31, 2024.
Katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 18 Agosti, 2024 katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Jijini Dar es Salaam, viongozi hao walipata nafasi ya kupitishwa katika mfumo wa Taifa wa kubadilishana taarifa uliojengwa na vijana wa Tanzania kwa kuzingatia usalama, uharaka, na misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi.
Mfumo huo uliwavutia viongozi kwa teknolojia iliyotumika, na unategemewa kumaliza changamoto ya mifumo kusomana na kubadilishana taarifa kwa haraka ikiwemo taarifa zinazotumwa nje ya nchi.
Viongozi waliohudhuria kikao hicho kilichoratibiwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Bw. Emmanuel Mkilia, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt. Nkundwe Mwasaga, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar Bw. Said Seif Said na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Dkt. Godwill Wanga.
Wengine walioshiriki kikao hicho ni maafisa waandamizi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali.
PDPC AND TIRA TO BUILD SUSTAINABLE…
IN DIGITAL ECONOMY PRIVACY SHOULD …
CONTACT US
Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Masha…
ULINZI WA TAARIFA BINAFSI UNAANZA …
JAMII YASHAURIWA KULINDA TAARIFA B…
PDPC KUSHIRIKIANA NA WADAU KUIMARI…
PDPC NA HILTON LAW GROUP WAKUTANA …
TUZINGATIE KANUNI ZA DHANA YA ULIN…