KILA TAASISI IWE NA SERA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

Aug. 9, 2024, 1:33 p.m. KILA TAASISI IWE NA SERA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

Taasisi za Umma na Binafsi nchini zinazokusanya au kuchakata Taarifa zimekumbushwa kuwa na Sera itakayo linda Taarifa Binafsi za watu kwa mujibu wa Sheria na kanuni za Ulinzi wa Taarifa Binafsi namba 11 ya mwaka 2022.

Akizungumza Jijini Mwanza kwenye kipindi cha DRIVE MIX kinachorushwa mbashara na JEMBE FM, Bw. Innocent Mungy, Mkuu wa Uhusiano na Mahusiano - Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) amesema kila Taasisi inayokusanya au kuchakata Taarifa nchini inapaswa kuwa na Sera ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ili kulinda Faragha za wateja.

“Kila Taasisi ya umma au binafsi inapaswa iwe na Sera inayoonesha jinsi watakavyokuwa wanalinda Taarifa Binafsi” Amesema Bw. Mungy

Katika hatua nyingine Bw. Mungy ametoa wito kwa Taasisi hizo kujisajili kwenye Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kabla ya tarehe 31 mwezi wa 12 mwaka huu kama alivyoagiza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akizindua PDPC mnamo April 3, mwaka huu.