BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI PDPC

Aug. 14, 2025, 3:55 p.m. BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI PDPC

Bodi ya Wakurugenzi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imefanya kikao chake cha sita ili kujadili utendaji kazi wa PDPC kwa kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni, 2025.

Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 14, 2025 jijini Dodoma na kimeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe. Balozi Adadi Rajabu, ambapo ametoa pongezi kwa niaba ya Wajumbe wa Bodi kwa mwelekeo mzuri na mafanikio ya PDPC ambayo yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake.

Aidha Balozi Adadi alitoa wito kwa timu ya Menejimenti ya PDPC kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano baina yao na watumishi ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Tanzania Census 2022