DPIA NI LAZIMA, KABLA YA KUANZISHA MRADI UNAOKUSANYA NA KUCHAKATA TAARIFA BINAFSI NCHINI
June 23, 2025, 8 p.m.
Mkurugenzi wa Tafiti za Ulinzi wa Taarifa na Teknolojia, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) -Dkt. Noe Nnko amezitaka Taasisi zote nchini kuhakikisha wanafanya Tathmini ya Athari za Ulinzi wa Taarifa (DPIA) kabla ya kuanzisha mradi wowote unaokusanya na kuchakata Taarifa Binafsi nchini.
Dkt. Noe amesema hayo leo Juni 23, 2025 jijini Arusha wakati akiwasilisha mada ya Kupunguza Madhara ya vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwenye Teknolojia zinazoibukia kwa washiriki wa mafunzo ya kupunguza madhara ya vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambapo amesema kufanya hivyo ni kutimiza moja ya takwa la Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44 ambayo imeipa Mamlaka PDPC kupitia DPIA za miradi yote inayohusisha Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi.
“Tunapaswa kufanya Tathmini ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPIA) kabla ya kuanzisha Mradi wowote nchini kwa mfano wale wanaofungua Viwanda hawawezi kufungua bila kushauriana au kuhakikiwa na NEMC vivyo hivyo huwezi kuanzisha Programu wezeshi yoyote (Application) bila kushauriana na PDPC kwakua Pragramu hiyo ikiwa na madhara kwenye Ulinzi wa Taarifa Binafsi haitaruhusiwa” amesema Dkt. Noe

PDPC TUNAHAKIKISHA ULINZI WA FARAG…

MSINGI WA UCHUMI WA KIDIJITALI UNA…

‘UNWANTED WITNESS’ WATEMBELEA PDPC

PDPC YASHIRIKI KIKAO - TATHMINI YA…

DKT. MKILIA AFUNGUA WARSHA JUKWAA …

PDPC Yatoa Mafunzo Maalumu kwa Bod…

ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIF…

PDPC YATOA ELIMU KWA UMMA MWANZA

ULINZI WA TAARIFA BINAFSI NI SWALA…

PDPC YATOA WITO WA USAJILI WA TAAS…

MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI NCHINI K…

PDPC YATANGAZA MAFUNZO KWA MAAFISA…

SIMAMIENI MIPANGO YA KUPUNGUZA VIH…

RISK CHAMPIONS NA DPO’s SHIRIKIANE…

WARATIBU NA WASIMAMIZI WA VIHATARI…

DPIA NI LAZIMA, KABLA YA KUANZISHA…

RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHUR…

TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES I…