DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

July 11, 2025, 3:55 p.m. DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

Leo Ijumaa tarehe 11/07/2025 Maafisa wa Ulinzi wa Taarifa (DPOs) kutoka taasisi za umma na binafsi wamepatiwa mafunzo ya kina kuhusu namna ya kufanya Tathmini ya Athari za Ulinzi wa Taarifa (DPIA) ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usimamizi na ulinzi wa taarifa binafsi katika taasisi zao.

Mafunzo hayo ya siku tatu (3) yaliyoandaliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Morena, Morogoro yakilenga kuwajengea uwezo maafisa ulinzi wa taarifa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi kwa mujibu wa sheria na kanuni za ulinzi wa taarifa binafsi nchini.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Bw. Nsaa-Iya Kihunrwa amesisitiza umuhimu wa DPIA kama nyenzo muhimu katika kutambua na kupunguza athari kabla ya kuanzishwa kwa mfumo au mradi unaohusisha uchakataji wa taarifa binafsi wakati wa utekelezaji wake.

“DPIA ni mchakato wa lazima kwa taasisi zote zinazochakata taarifa binafsi. Kwa kufanya tathmini hii mapema, tunalinda haki za msingi za watu kwenye taarifa zao binafsi na pia tunazuia madhara ya kisheria au ya kiutendaji kwa taasisi zetu,” alisema Bw. Kihunrwa.

Mafunzo haya ya siku tatu yamehitimishwa leo ambapo yalihusisha ufafanuzi wa kina juu ya majukumu ya maafisa ulinzi wa taarifa kwenye taasisi zao na washiriki walipata fursa ya kujadili visa halisi, kushiriki katika makundi ya kazi, na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa sheria na teknolojia ya habari kuhusu changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Mafunzo haya yanatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uelewa na utekelezaji wa Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi, sambamba na kuinua viwango vya ulinzi wa taarifa binafsi nchini.

RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHURUTI

RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHUR…

June 24, 2025, 2 p.m.
TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES IN UN CSTD MULTI-STAKEHOLDERS WORKING GROUP ON …

TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES I…

July 4, 2025, 8 a.m.
ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

July 2, 2025, 3:55 p.m.
𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐓𝐄𝐍𝐃𝐄𝐃 𝐓𝐇𝐄 𝐖𝐒𝐈𝐒+𝟐𝟎 𝐇𝐈𝐆𝐇-𝐋𝐄𝐕𝐄𝐋 𝐄𝐕𝐄𝐍𝐓 𝐈𝐍 𝐆𝐄𝐍𝐄𝐕𝐀

𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐓𝐄𝐍𝐃𝐄𝐃 𝐓𝐇𝐄 𝐖𝐒𝐈𝐒+𝟐𝟎 𝐇𝐈𝐆𝐇…

July 7, 2025, 9:05 a.m.
DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BINAFSI KWENYE TAASISI/KAMPUNI YAKO

DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BIN…

July 9, 2025, 5:26 p.m.
NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI WA TAARIFA KWENYE …

NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI W…

July 10, 2025, 3:54 p.m.
DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI W…

July 11, 2025, 3:55 p.m.
PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFISA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI NCHINI

PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFIS…

July 16, 2025, 3:07 p.m.
ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI YATOLEWA MAONESHO …

ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIF…

Aug. 10, 2025, 4:24 p.m.
BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI PDPC

BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BOD…

Aug. 14, 2025, 3:55 p.m.
JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWA WADAU KWA KULINDA TAARIFA …

JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWA…

Aug. 20, 2025, 8:57 p.m.
NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII …

NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU K…

Aug. 20, 2025, 8:58 p.m.
𝐊𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐋𝐈𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐁𝐈𝐍𝐀𝐅𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈 𝐍𝐈 …

𝐊𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐋𝐈𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 …

Aug. 21, 2025, 2:38 p.m.
𝐔𝐒𝐈𝐖𝐄𝐊𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐓𝐔 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐌𝐃𝐇𝐀𝐌𝐈𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐎 𝐁𝐈𝐋𝐀 𝐊𝐔𝐏𝐀𝐓𝐀 𝐑𝐈𝐃𝐇𝐀𝐀 …

𝐔𝐒𝐈𝐖𝐄𝐊𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐓𝐔 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐌𝐃𝐇𝐀𝐌𝐈…

Aug. 21, 2025, 2:46 p.m.
KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA NCHI NI LAZIMA KUPATA KIBALI …

KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA…

Aug. 22, 2025, 4:45 p.m.
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA BINAFSI ZA WATU

KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAG…

Sept. 5, 2025, 8:53 a.m.
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA BINAFSI UNAJENGA IMANI YA WANANCHI …

ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA B…

Sept. 11, 2025, 11:23 a.m.
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikiano katika Kulinda Faragha na Taarifa …

PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikian…

Nov. 12, 2025, 6:56 p.m.
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA YAWAFIKIA PDPC

ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RU…

Nov. 24, 2025, 10:12 p.m.
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA ULINZI WA TAARIFA

DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGE…

Dec. 4, 2025, 7:08 p.m.