DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA ULINZI WA TAARIFA
Dec. 4, 2025, 7:08 p.m.
Washiriki wa mafunzo maalum ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa (DPOs) wameipongeza Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kwa kuandaa na kutoa mafunzo mahususi yanayolenga kuwaongezea uwezo kwenye utendaji wao hasa katika kusimamia na kulinda taarifa binafsi ndani ya taasisi zao.
Wamesema mafunzo hayo yamewajengea uelewa wa kina kuhusu matakwa ya sheria, mbinu za kutathmini athari, na namna ya kuhakikisha taarifa za wananchi zinalindwa ipasavyo katika mfumo wa kidigitali unaokua kwa kasi.
“Mafunzo haya binafsi yamenifungua macho kuhusu umuhimu wa kuwa na mifumo madhubuti ya ulinzi wa taarifa tulizonazo kwenye kampuni yetu, na yametupa weledi wa jinsi ya kusimamia mzunguko mzima wa taarifa kuanzia ukusanyaji hadi uhifadhi. Nawapongeza sana PDPC, utayari wao wa kutoa mafunzo ya mara kwa mara ni ishara ya kujitoa katika kuhakikisha taifa linakuwa na wataalamu wenye uwezo wa kutosha kulinda taarifa binafsi’’ amesema Bw. Enock Helongwa, DPO - Taasa Luxurious Lodges & Camps.
“Naishauri PDPC kuendeleza utaratibu huu wa utoaji wa mafunzo ili kuwafikia Maafisa Ulinzi wa Taarifa wengi zaidi kwa sababu ulinzi wa taarifa binafsi ni eneo linalohitaji uelewa mpana ndani ya taasisi zote, bila kujali ukubwa au aina ya huduma inayotolewa” amesema Bi. Margaret Mhina, DPO - C. Steinweg Bridge Tanzania Limited.
Mafunzo hayo ya siku tatu kwa Maafisa Ulinzi wa Taarifa (DPOs) yanalenga kuhakikisha kila taasisi nchini inakuwa na DPO mwenye ujuzi wa kutosha kutekeleza misingi ya ulinzi wa taarifa kwa kuzingatia haki, uwazi, usalama na uwajibikaji. Mafunzo yamekuwa endelevu ikiwa hii ni awamu ya tano ambapo zaidi ya DPOs 200 wameweza kushiriki hivyo kuongeza idadi ya wataalamu wanaobobea katika fani hiyo muhimu.
RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHUR…
TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES I…
ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO
𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐓𝐄𝐍𝐃𝐄𝐃 𝐓𝐇𝐄 𝐖𝐒𝐈𝐒+𝟐𝟎 𝐇𝐈𝐆𝐇…
DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BIN…
NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI W…
DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI W…
PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFIS…
ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIF…
BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BOD…
JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWA…
NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU K…
𝐊𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐋𝐈𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 …
𝐔𝐒𝐈𝐖𝐄𝐊𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐓𝐔 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐌𝐃𝐇𝐀𝐌𝐈…
KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA…
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAG…
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA B…
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikian…
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RU…
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGE…