ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA YAWAFIKIA PDPC
Nov. 24, 2025, 10:12 p.m.
Afisa uelimishaji kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw. Faustine Malecha leo Jumatatu tarehe 24 Novemba, 2025 ametoa elimu kwa watumishi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kuhusu umuhimu wa kuzuia na kuepuka vitendo vya rushwa katika maeneo ya kazi.
Katika mafunzo hayo, yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za PDPC, zilizopo Dodoma, Bw. Malecha amesisitiza kuwa rushwa si tu inashusha ufanisi wa taasisi za umma, bali pia inaathiri uaminifu wa wananchi kwa Serikali na kuhatarisha maendeleo ya Taifa.
“PDPC ni taasisi muhimu inayosimamia utekelezaji wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi, inapaswa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kuhakikisha kuwa maamuzi yote yanafanywa kwa uadilifu, uwazi na haki” amesema Bw. Malecha.
Bw. Malecha pia alitoa mwongozo wa namna watumishi wanaweza kutambua viashiria vya rushwa, jinsi ya kuripoti vitendo vinavyohisiwa kuwa ni vya rushwa, na umuhimu wa kujenga utamaduni wa kuwajibika katika kila hatua ya utoaji huduma.
PDPC ina jukumu la msingi la kulinda haki ya faragha ya wananchi kwa kuhakikisha taarifa zao binafsi zinakusanywa, kuhifadhiwa na kutumika kwa mujibu wa sheria hivyo kujenga jamii inayotumia teknolojia kwa usalama, uaminifu na kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAG…
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA B…
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikian…
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RU…
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGE…
KARIBU PDPC MHE. ANGELLAH JASMINE …
KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUG…
PDPC AND HUAWEI HOST PRIVACY PROTE…
MINISTER KAIRUKI ISSUES FINAL THRE…
𝐓𝐀𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐎𝐓𝐄 𝐍𝐂𝐇𝐈𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐙𝐈𝐌𝐀 𝐊𝐔𝐖𝐀…
𝐊𝐔𝐓𝐎𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐓𝐀𝐊𝐖𝐀 𝐘𝐀 𝐏𝐃𝐏𝐀 𝐍𝐈 𝐇𝐀…
PDPC YATOA ELIMU YA DHANA YA ULINZ…