KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA BINAFSI ZA WATU

Sept. 5, 2025, 8:53 a.m. KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA BINAFSI ZA WATU

Mkurugenzi Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Ofisi ya Zanzibar, Bi Rehema Abdalla amewataka wagombea wa ngazi zote nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kuhakikisha hawaingilii faragha za watu.


Bi. Rehema amezungumza hayo wakati akifanya mahojiano maalum na mtangazaji Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bi. Nasra Khatib kuhusu umuhimu wa kulinda taarifa binafsi katika kampeni za uchaguzi mkuu kwa wagombea watakaonadi sera za vyama vyao.

“Wagombea wa ngazi zote hakikisheni hamuingilii faragha za watu na majukwaa mnayotumia kunadi sera za vyama vyenu yasitumike kukiuka misingi ya Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi” amesema Bi. Rehema.

Akisisitiza swala hili, Bi. Rehema amesema kuwa kuchapisha taarifa binafsi za mtu kwenye magazeti, mitandao ya kijamii au kutangaza kwenye redio na televisheni bila ridhaa ya muhusika wa taarifa hizo ni kinyume na matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi sura ya 44.

Elimu juu ya dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa makundi mbalimbali ya kijamii ni endelevu na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inatoa elimu hiyo kuwajengea uelewa wahusika wa taarifa binafsi na watumiaji wa taarifa hizo ili uzingatiaji wa ulinzi wa faragha upewe kipaumbele wakati wa kutumia taarifa husika.

Tanzania Census 2022