KIKAO KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU

Jan. 22, 2025, 4:11 p.m. KIKAO KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Moshi Kakoso, akiiongoza kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge na taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai-Disemba 2024), Januari 20, 2025, Bungeni jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa PDPC Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia anashiriki katika Mkutano huo pamoja na viongozi wengine wa PDPC akiwemo Meneja wa Huduma Saidizi wa PDPC Dkt. Petro Nzowa na Mwanasheria wa PDPC Bw. Osiniel Mfinanga.