πππππππ ππππ ππ ππππππ ππ ππππππ π πππππ ππ ππππππ πππππππ ππ ππππππ ππ πππ
Aug. 21, 2025, 2:38 p.m.
Kwa mujibu wa Kanuni za Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi za mwaka 2023, kuandaa Sera ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mkusanyaji na Mchakataji wa Taarifa ni moja ya jukumu la msingi la Afisa Ulinzi wa Taarifa (DPO).
Mtaalamu wa Masuala ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Bi. Asha Sinare, amesema hayo leo Agosti 21, 2025 wakati akitoa mada kwenye Mafunzo Maalumu ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa yanayoendelea hapa Mjini Morogoro ambapo amesema wapo baadhi ya DPO's wanakwepa jukumu hilo na kuwaachia wanasheria wa Taasisi au kampuni husika.
"Kuandaa Sera ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Taasisi au kampuni ni moja ya jukumu la msingi la DPO, najua wapo baadhi yenu wanakwepa jukumu hili na kuwapa wanasheria ila niwaambie tu hili ni jukumu la DPO na ukiwa unaiandaa ni vizuri ukawashirikisha watumishi wa kila idara kwenye Taasisi yako ili uweze kuandaa Sera nzuri inayoendana na utendaji kazi na majukumu ya Taasisi husika". Amesema Bi. Sinare
"Kifungu cha 32 cha Kanuni za Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi za mwaka 2023 kimeainisha majukumu ya DPO's ikiwemo kufanya Tathimini ya Athari za Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPIA) na kutayarisha ripoti za kila robo mwaka." Aliongeza Bi.Sinare
Aidha Bi.Sinare aliwashauri DPO's hao kuwa na utaratibu wa kufanya ukaguzi wa ndani juu ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi sambamba na kuandaa orodha ya mambo yatakayokaguliwa ili kutimiza majukumu yao kwa weledi.

SIMAMIENI MIPANGO YA KUPUNGUZA VIHβ¦

RISK CHAMPIONS NA DPOβs SHIRIKIANEβ¦

WARATIBU NA WASIMAMIZI WA VIHATARIβ¦

DPIA NI LAZIMA, KABLA YA KUANZISHAβ¦

RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHURβ¦

TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES Iβ¦

ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

ππππππππ ππππππππ πππ ππππ+ππ ππππβ¦

DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BINβ¦

NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI Wβ¦

DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI Wβ¦

PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFISβ¦

ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIFβ¦

BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODβ¦

JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWAβ¦

NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU Kβ¦

πππππππ ππππ ππ ππππππ ππ ππππππ π β¦

πππππππ ππππππ π ππ πππ ππππ ππππππβ¦

KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YAβ¦
.
