KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA NCHI NI LAZIMA KUPATA KIBALI PDPC

Aug. 22, 2025, 4:45 p.m. KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA NCHI NI LAZIMA KUPATA KIBALI PDPC

Taarifa Binafsi yoyote inayoenda nje ya nchi ni lazima ipatiwe kibali na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC).

Haya yamesemwa leo Agosti 22,2025, Morogoro Mjini na Bw. Innocent Mungy, Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano - PDPC wakati akitoa mada ya namna ya kuomba kibali cha kusafirisha Taarifa Nje ya Nchi kwenye Mafunzo Maalumu ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa (DPO) ambapo amesema hilo ni takwa la Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 hivyo Taasisi, kampuni au mtu yoyote anaesafirisha Taarifa Binafsi nje ya Mipaka ya Tanzania anapaswa kuomba kibali PDPC.

"Hata wale wanaosafirisha Taarifa Binafsi kwaajili ya kwenda kuzitunza mtandaoni 'Cloud Server' wanapaswa kupewa kibali na PDPC na wakati wa kuomba kibali hicho wanatakiwa kusema hiyo 'server' ipo nchi gani, mtoa huduma ni nani na ni taarifa zipi wanazozisafirisha" Amesema Bw.Mungy
 

Tanzania Census 2022