ππππππππππππ πππππππ ππ ππππ ππ ππππππ πππ π ππππππ, πππππππ ππ ππππ ππ ππππππππ
Feb. 11, 2026, 2:01 p.m.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia amesema kuwa kutotekeleza matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPA) ni hatari kwa faragha, usalama na haki za wananchi.
Hayo yamesemwa leo Februari 11, 2026 katika mafunzo maalum ya maafisa ulinzi wa taarifa binafsi awamu ya saba, yaliyofanyika katika ukumbi wa City Park Garden jijini Mbeya akiwa anazungumza na washiriki hao.
βTume imebaini baadhi ya taasisi kutokua tayari kikamilifu kutekeleza matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, hususan katika usajili na uteuzi wa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Baadhi ya taasisi zinaendelea kukusanya na kuchakata taarifa binafsi bila kukamilisha matakwa ya kisheriaβ
βLengo la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa ukusanyaji, uchakataji, uhifadhi na matumizi ya taarifa binafsi vinafanyika kwa kuzingatia kikamilifu matakwa ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi. Hivyo kupitia mafunzo haya tunatarajia kuona mabadiliko ya vitendo katika taasisi zinazoshiriki mafunzo hayaβ amesema Dkt. Mkilia.
Dkt. Mkilia amesisitiza kuwa PDPC imejipanga kuanza ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria, kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya usajili na uteuzi wa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi, na kuchukua hatua za kisheria pale ambapo kutabainika ukiukwaji.
Mafunzo haya ya siku tatu kwa maafisa ulinzi wa taarifa binafsi yanafanyika hapa jiini Mbeya kuanzia leo Februari 11, 2026 ikiwa ni awamu ya saba ya mafunzo hayo, kwa kipindi hiki yakilenga taasisi za umma na binafsi zilizopo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODβ¦
πππππππ ππππππ π ππ πππ ππππ ππππππβ¦
KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YAβ¦
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAGβ¦
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA Bβ¦
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikianβ¦
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUβ¦
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGEβ¦
KARIBU PDPC MHE. ANGELLAH JASMINE β¦
KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUGβ¦
PDPC AND HUAWEI HOST PRIVACY PROTEβ¦
MINISTER KAIRUKI ISSUES FINAL THREβ¦
πππππππ ππππ ππππππ ππ ππππππ ππππβ¦
ππππππππππππ πππππππ ππ ππππ ππ ππβ¦