PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikiano katika Kulinda Faragha na Taarifa Binafsi za Wanachama

Nov. 12, 2025, 6:56 p.m. PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikiano katika Kulinda Faragha na Taarifa Binafsi za Wanachama

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Mkilia, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka, jijini Dodoma. 

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili katika kulinda faragha na taarifa binafsi za wanachama wa NHIF, hasa katika zama hizi za mabadiliko ya kidijitali katika utoaji wa huduma za afya.

Kupitia Sheria ya Bima ya Afya ya Taifa, NHIF ina jukumu muhimu la kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma bora na nafuu za afya. Mfuko huo unasimamia taarifa nyeti binafsi za kiafya za mamilioni ya wananchi, hivyo usalama na uadilifu wa taarifa hizo ni msingi wa kuimarisha imani ya umma katika mifumo ya kidijitali.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mkilia amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya PDPC na NHIF ni muhimu katika kuhakikisha usimamizi wa taarifa binafsi unafanyika kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa vya faragha na usalama wa taarifa. Aliongeza kuwa juhudi za pamoja zitasaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za faragha na wajibu wa kulinda taarifa zao wanapotumia huduma za bima ya afya.

Kwa upande wake, Dkt. Isaka ameeleza kuwa NHIF inatekeleza mageuzi makubwa ya kidijitali yanayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma, na kwamba ushirikiano na PDPC utasaidia kuhakikisha mifumo hiyo ni salama na inalindwa na kuaminika zaidi.

Viongozi hao wamekubaliana kuwa na mpango wa pamoja wa uelimishaji wa umma. PDPC na NHIF zitashirikiana kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda taarifa zao binafsi za kiafya kupitia bima ya afya na umuhimu wa kujua hatima ya faragha za taarifa hizo. 

Ushirikiano huu utasaidia kuimarisha imani ya wananchi katika mifumo ya afya na taarifa katika mifumo ya kidijitali; Kukuza uwajibikaji katika usimamizi wa taarifa binafsi kwa watoa huduma na wanufaika; Kusaidia utekelezaji wa ajenda ya Serikali kuhusu bima ya afya kwa wote; kuongeza uelewa na utii wa sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44 na zile za kimataifa kuhusu faragha na ulinzi wa taarifa binafsi.

Ushirikiano huu kati ya PDPC na NHIF unatarajiwa kuwa mfano wa kuigwa katika sekta ya afya na taasisi nyingine za umma na binafsi, katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kwa usalama, uwazi na uaminifu katika matumizi ya teknolojia za kidijitali katika huduma za afya zenye taarifa nyeti za wanachama.

RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHURUTI

RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHUR…

June 24, 2025, 2 p.m.
TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES IN UN CSTD MULTI-STAKEHOLDERS WORKING GROUP ON …

TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES I…

July 4, 2025, 8 a.m.
ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

July 2, 2025, 3:55 p.m.
𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐓𝐄𝐍𝐃𝐄𝐃 𝐓𝐇𝐄 𝐖𝐒𝐈𝐒+𝟐𝟎 𝐇𝐈𝐆𝐇-𝐋𝐄𝐕𝐄𝐋 𝐄𝐕𝐄𝐍𝐓 𝐈𝐍 𝐆𝐄𝐍𝐄𝐕𝐀

𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐓𝐄𝐍𝐃𝐄𝐃 𝐓𝐇𝐄 𝐖𝐒𝐈𝐒+𝟐𝟎 𝐇𝐈𝐆𝐇…

July 7, 2025, 9:05 a.m.
DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BINAFSI KWENYE TAASISI/KAMPUNI YAKO

DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BIN…

July 9, 2025, 5:26 p.m.
NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI WA TAARIFA KWENYE …

NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI W…

July 10, 2025, 3:54 p.m.
DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI W…

July 11, 2025, 3:55 p.m.
PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFISA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI NCHINI

PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFIS…

July 16, 2025, 3:07 p.m.
ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI YATOLEWA MAONESHO …

ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIF…

Aug. 10, 2025, 4:24 p.m.
BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI PDPC

BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BOD…

Aug. 14, 2025, 3:55 p.m.
JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWA WADAU KWA KULINDA TAARIFA …

JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWA…

Aug. 20, 2025, 8:57 p.m.
NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII …

NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU K…

Aug. 20, 2025, 8:58 p.m.
𝐊𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐋𝐈𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐁𝐈𝐍𝐀𝐅𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈 𝐍𝐈 …

𝐊𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐋𝐈𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 …

Aug. 21, 2025, 2:38 p.m.
𝐔𝐒𝐈𝐖𝐄𝐊𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐓𝐔 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐌𝐃𝐇𝐀𝐌𝐈𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐎 𝐁𝐈𝐋𝐀 𝐊𝐔𝐏𝐀𝐓𝐀 𝐑𝐈𝐃𝐇𝐀𝐀 …

𝐔𝐒𝐈𝐖𝐄𝐊𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐓𝐔 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐌𝐃𝐇𝐀𝐌𝐈…

Aug. 21, 2025, 2:46 p.m.
KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA NCHI NI LAZIMA KUPATA KIBALI …

KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA…

Aug. 22, 2025, 4:45 p.m.
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA BINAFSI ZA WATU

KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAG…

Sept. 5, 2025, 8:53 a.m.
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA BINAFSI UNAJENGA IMANI YA WANANCHI …

ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA B…

Sept. 11, 2025, 11:23 a.m.
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikiano katika Kulinda Faragha na Taarifa …

PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikian…

Nov. 12, 2025, 6:56 p.m.
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA YAWAFIKIA PDPC

ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RU…

Nov. 24, 2025, 10:12 p.m.
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA ULINZI WA TAARIFA

DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGE…

Dec. 4, 2025, 7:08 p.m.