PDPC YATOA ELIMU KWA UMMA MWANZA

March 21, 2025, 8 p.m. PDPC YATOA ELIMU KWA UMMA MWANZA

Timu ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Emmanuel Mkilia wamefika Studio za Star Tv kwa lengo la kutoa elimu kwa Umma kuhusu Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Akizungumza katika Studio hizo kupitia kipindi cha Tuongee Asubuhi Dkt. Mkilia ametoa wito kwa Taasisi zinazokusanya na kuchakata Taarifa Binafsi nchini kujisajili kwenye Mfumo wa Usajili PDPC kabla ya April 30, 2025 ili kutimiza matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Namba 11 ya Mwaka 2022, Sura ya 44.

Kwa Upande wake Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano - PDPC, Bw. Innocent Mungy amesema PDPC imeweka Kambi jijini Mwanza ili kuhakikisha Elimu ya Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inawafikia wakazi wote wa eneo hilo ikiwa ni utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo aliitaka Tume kuielimisha jamii kuhusu Ulinzi wa Taarifa Binafsi