PDPC YATOA ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI KWA WAFANYA BIASHARA MKOA WA NJOMBE
Feb. 17, 2026, 8:28 p.m.
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imeendelea kuimarisha uelewa wa wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa ulinzi wa faragha na taarifa binafsi, wakati wa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Biashara Mkoa wa Njombe uliofanyika Februari 17, 2026 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Akitoa elimu hiyo, Mkuu wa Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano wa PDPC Bw. Innocent Mungy, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu PDPC Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, amefikisha salamu na pongezi kwa wafanyabiashara wa mkoa huo kwa mchango wao katika kukuza uchumi wa taifa na kuwasisitiza kuwa ulinzi wa taarifa binafsi si suala la kisheria pekee, bali ni msingi wa uaminifu katika biashara za kisasa.
“Haki ya faragha ni haki ya msingi ya binadamu inayolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na biashara yoyote inayokusanya au kuchakata taarifa binafsi ina wajibu wa kuzilinda kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 ambayo ni sehemu ya mfumo wa sheria pacha tatu za uchumi wa kidijitali zinazojumuisha Sheria ya Miamala ya Kielektroniki na Sheria ya Usalama Mtandao, ambazo kwa pamoja zinajenga mazingira salama na yenye uaminifu kwa biashara na huduma za kidijitali” amesema Bw. Mungy.
Wafanyabiashara hao wametakiwa kuzingatia misingi ya ulinzi wa taarifa, ikiwemo kukusanya taarifa zinazohitajika tu, kuzilinda dhidi ya uvujaji, kuzitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa, na kuwapa wafanyakazi wao elimu kuhusu wajibu wa kulinda taarifa za wateja.
PDPC inaendelea kuwakumbusha wafanyabiashara wote kuwa muda wa nyongeza wa usajili wa hiari kwa taasisi na biashara zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi unaisha tarehe 8 Aprili 2026, na baada ya hapo Tume itaanza ukaguzi wa utekelezaji wa sheria kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali, hivyo watumie muda uliobaki kujisajili, kuboresha mifumo yao ya ulinzi wa taarifa, na kujenga biashara zinazolinda faragha, uaminifu na ushindani katika soko la kisasa la kidijitali.
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAG…
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA B…
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikian…
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RU…
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGE…
KARIBU PDPC MHE. ANGELLAH JASMINE …
KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUG…
PDPC AND HUAWEI HOST PRIVACY PROTE…
MINISTER KAIRUKI ISSUES FINAL THRE…
𝐓𝐀𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐎𝐓𝐄 𝐍𝐂𝐇𝐈𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐙𝐈𝐌𝐀 𝐊𝐔𝐖𝐀…
𝐊𝐔𝐓𝐎𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐓𝐀𝐊𝐖𝐀 𝐘𝐀 𝐏𝐃𝐏𝐀 𝐍𝐈 𝐇𝐀…
PDPC YATOA ELIMU YA DHANA YA ULINZ…