RISK CHAMPIONS NA DPO’s SHIRIKIANENI KULINDA TAARIFA BINAFSI NCHINI

June 23, 2025, 7:18 p.m. RISK CHAMPIONS NA DPO’s SHIRIKIANENI KULINDA TAARIFA BINAFSI NCHINI

Waratibu na Wasimamizi wa Vihatarishi (Risk Champions) wakishirikiana na Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPO's) wakifanyakazi kwa ushirikiano itarahisisha Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwenye Taasisi husika. 


Hayo yamesemwa na Mhandisi Stephen Wangwe, Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji, Tume ya Ulinzi waTaarifa Binafsi (PDPC)  jijini Arusha wakati akiwasilisha mada ya Wasilisho la Ulinzi wa Taarifa Binafsi Tanzania kwa Muhtasari, kwa washiriki wa mafunzo ya kupunguza madhara ya vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambapo amesema ili kupata matokeo chanya katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi Nchini, inapaswa Risk Champions na DPO’s washirikiane kikamilifu kupunguza madhara ya vihatarishi vya Ulinzi wa Taarifa kwenye Taasisi zao.

Mafunzo haya ya siku tatu yaliyoanza tarehe 23 Juni, 2025 yanahusisha Waratibu na Wasimamizi wa Vihatarishi, Wajumbe wa Bodi,Wakuu wa Idara au Vitengo, Maafisa Tehama na Wakaguzi wa Ndani na Nje.