ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

July 2, 2025, 3:55 p.m. ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

Zoezi la kutoa Elimu ya Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Umma linaendelea kutolewa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), ambapo leo Julai 02, 2025 Mkoani Morogoro zaidi ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPO’s) Mia nne(400) wamepatiwa elimu hiyo kupitia Semina Maalumu iliyobebwa na ujumbe wa Kuwezesha Uzingatiaji wa Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi Nchini.

Bw. Innocent Mungy, Mkuu wa Kitengo Uhusiano na Mawasiliano PDPC na mmoja wa wakufunzi wa Mafunzo haya Maalumu kwa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi ametumia jukwaa hili kuwashauri maafisa hao kuweka utaratibu wa kutunza kumbukumbu za Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa kwenye Taasisi zao ili kutimiza majukumu yao kwa Usahihi.

Akiwafundisha maafisa hao Bw.Mungy amesema Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi sura ya 44 (PDPA) na kanuni zake, zimetungwa ili kuleta uwazi na uwajibikaji kwa Taasisi pale linapokuja suala la Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi hivyo DPO anapaswa kutumia mfumo wa ROPA kutimiza malengo hayo.

“ROPA ni kitendo  cha kuweka kumbukumbu ya shughuli zote za Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi na hii ni moja ya njia bora ya kutimiza majukumu yako kama DPO kwakua hata itakapotokea Taarifa zimevuja ni rahisi kujua tatizo lilianzia wapi na ukalitatua” amesema Bw. Mungy