ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO
July 2, 2025, 3:55 p.m.
Zoezi la kutoa Elimu ya Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Umma linaendelea kutolewa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), ambapo leo Julai 02, 2025 Mkoani Morogoro zaidi ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPO’s) Mia nne(400) wamepatiwa elimu hiyo kupitia Semina Maalumu iliyobebwa na ujumbe wa Kuwezesha Uzingatiaji wa Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi Nchini.
Bw. Innocent Mungy, Mkuu wa Kitengo Uhusiano na Mawasiliano PDPC na mmoja wa wakufunzi wa Mafunzo haya Maalumu kwa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi ametumia jukwaa hili kuwashauri maafisa hao kuweka utaratibu wa kutunza kumbukumbu za Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa kwenye Taasisi zao ili kutimiza majukumu yao kwa Usahihi.
Akiwafundisha maafisa hao Bw.Mungy amesema Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi sura ya 44 (PDPA) na kanuni zake, zimetungwa ili kuleta uwazi na uwajibikaji kwa Taasisi pale linapokuja suala la Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi hivyo DPO anapaswa kutumia mfumo wa ROPA kutimiza malengo hayo.
“ROPA ni kitendo cha kuweka kumbukumbu ya shughuli zote za Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi na hii ni moja ya njia bora ya kutimiza majukumu yako kama DPO kwakua hata itakapotokea Taarifa zimevuja ni rahisi kujua tatizo lilianzia wapi na ukalitatua” amesema Bw. Mungy

SIMAMIENI MIPANGO YA KUPUNGUZA VIH…

RISK CHAMPIONS NA DPO’s SHIRIKIANE…

WARATIBU NA WASIMAMIZI WA VIHATARI…

DPIA NI LAZIMA, KABLA YA KUANZISHA…

RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHUR…

TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES I…

ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐓𝐄𝐍𝐃𝐄𝐃 𝐓𝐇𝐄 𝐖𝐒𝐈𝐒+𝟐𝟎 𝐇𝐈𝐆𝐇…

DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BIN…

NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI W…

DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI W…

PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFIS…

ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIF…

BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BOD…

JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWA…

NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU K…

𝐊𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐋𝐈𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 …

𝐔𝐒𝐈𝐖𝐄𝐊𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐓𝐔 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐌𝐃𝐇𝐀𝐌𝐈…

KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA…
.
