ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA BINAFSI UNAJENGA IMANI YA WANANCHI KWA TAASISI
Sept. 11, 2025, 11:23 a.m.
Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Ofisi ya Zanzibar Bi. Rehema Abdalla ameukumbusha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kuendelea kutunza faragha za taarifa za wateja wao kwa kuhakikisha wanatumia taarifa wanazozikusanya au kuzichakata kwa misingi inayokusudiwa tu.
Bi. Rehema ameyasema hayo katika mafunzo ya siku moja kwa watumishi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Ofisi ya Zanzibar yaliyotolea na Afisa wa PSSSF Bw. Seif Khamis yakilenga kuwajengea uelewa watumishi hao juu ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma.
“Ninausifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma kwa kutumia teknolojia mpya inayorahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja. Nawasihi katika utekelezaji wa shughuli zenu kuzingatia faragha katika kukusanya na kuchakata taarifa za wateja wenu ili kujenga imani kwa wanachama wa mfuko huo” amesema Bi. Rehema
Msisitizo wa ulinzi wa faragha za taarifa za watu ni njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuhakikisha taasisi zote za umma na binafsi zinazingatia kanuni za ulinzi wa faragha, ili kujenga imani ya wananchi katika mifumo ya kidigitali.
BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BOD…
𝐔𝐒𝐈𝐖𝐄𝐊𝐄 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐓𝐔 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐌𝐃𝐇𝐀𝐌𝐈…
KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YA…
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAG…
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA B…
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikian…
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RU…
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGE…
KARIBU PDPC MHE. ANGELLAH JASMINE …
KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUG…
PDPC AND HUAWEI HOST PRIVACY PROTE…
MINISTER KAIRUKI ISSUES FINAL THRE…
𝐓𝐀𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐎𝐓𝐄 𝐍𝐂𝐇𝐈𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐙𝐈𝐌𝐀 𝐊𝐔𝐖𝐀…
𝐊𝐔𝐓𝐎𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐓𝐀𝐊𝐖𝐀 𝐘𝐀 𝐏𝐃𝐏𝐀 𝐍𝐈 𝐇𝐀…