πππππππ ππππππ π ππ πππ ππππ ππππππππ ππππ ππππ ππππππ ππππππ ππππ
Aug. 21, 2025, 2:46 p.m.
Ni kosa kisheria kuweka Taarifa za mtu kama mdhamini wako bila kupata ridhaa yake.
Haya yamesemwa leo Agosti 21,2025 na Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Mhandisi Stephen Wangwe Β wakati akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa (DPOs) yanayoendelea hapa mjini Morogoro.Β
Mhandisi wangwe amesema kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 (PDPA) ni kosa kutumia taarifa yoyote ya mtu bila ridhaa yake. Hivyo hata wale wanaoweka taarifa za watu kama wadhamini wao bila kupata ridhaa wanaenda kinyume na Sheria.
"Kuna baadhi wa watu kwenye jamii wanaandika taarifa za wadhamini sehemu mbalimbali bila kuomba ridhaa za wahusika. Mfano kwenye barua za maombi ya kazi au kwenye maombi ya mkopo, hii ni kinyume na sheria na haipaswi kuwa hivyo" Amesema Mhandisi WangweΒ
Akijibu swali lingine kuhusu baadhi ya watafiti wanaokusanya na kuchakata taarifa nyeti za watu bila kupata ridhaa, Mhandisi wangwe amesema wakusanyaji na wachakataji wa taarifa wanapokua kwenye majukumu yao ya kikazi wanapaswa kuzingatia haki za muhusika wa taarifa Β kwakua PDPA ipo kumlinda muhusika wa taarifa.
Zaidi ya DPO's 200 kutoka ndani na nje ya nchi wameshiriki kwenye awamu hii ya nne ya mafunzo maalumu ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa ambayo yameanza Agosti 20 na yatafikia tamati Agosti 22, 2025.

SIMAMIENI MIPANGO YA KUPUNGUZA VIHβ¦

RISK CHAMPIONS NA DPOβs SHIRIKIANEβ¦

WARATIBU NA WASIMAMIZI WA VIHATARIβ¦

DPIA NI LAZIMA, KABLA YA KUANZISHAβ¦

RIDHAA INAPASWA KUTOLEWA BILA SHURβ¦

TANZANIA DELEGATION PARTICIPATES Iβ¦

ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO

ππππππππ ππππππππ πππ ππππ+ππ ππππβ¦

DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BINβ¦

NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI Wβ¦

DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI Wβ¦

PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFISβ¦

ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIFβ¦

BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODβ¦

JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWAβ¦

NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU Kβ¦

πππππππ ππππ ππ ππππππ ππ ππππππ π β¦

πππππππ ππππππ π ππ πππ ππππ ππππππβ¦

KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YAβ¦
.
