WARATIBU NA WASIMAMIZI WA VIHATARISHI NCHINI TIMIZENI WAJIBU WENU

June 23, 2025, 6:28 p.m. WARATIBU NA WASIMAMIZI WA VIHATARISHI NCHINI TIMIZENI WAJIBU WENU

Waratibu na Wasimamizi wa Vihatarishi nchini wameshauriwa kuwaelimisha wafanyakazi wenzao namna ya kupunguza madhara ya Vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Wito huo umetolewa jijini Arusha leo Juni 23, 2025 na Bw. Innocent Mungy, Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) wakati akitoa mada ya Usimamizi wa Vihatarishi kwa washiriki wa mafunzo ya kupunguza madhara ya vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambapo amesema elimu hiyo ni muhimu ifike kwa watumishi wote wa Taasisi husika na hiyo ni moja ya jukumu la  waratibu na wasimamizi wa vihatarishi kwenye Taasisi hivyo watimize wajibu wao.

“Kama ilivyo PDPC ni jukumu letu kutoa elimu kwa umma kuhusu Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na nyinyi ni jukumu lenu kutoa elimu kwa Watumishi wenzenu juu ya namna ya kupunguza madhara ya vihatarishi kwenye Taasisi, kwahiyo timizeni wajibu wenu” amesema Bw. Mungy