JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWA WADAU KWA KULINDA TAARIFA ZAO BINAFSI
Aug. 20, 2025, 9:03 p.m.
Ikiwa ni siku ya kwanza ya awamu ya nne ya mafunzo maalum kwa Maafisa ulinzi wa Taarifa Binafsi kutoka kwenye taasisi za umma na binafsi nchini, maafisa hao wametakiwa kuhakikisha taarifa binafsi za wadau wa taasisi zao zinalindwa kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44.
Akitoa mafunzo hayo Bi. Hellen Achimpota leo tarehe 20 Agosti, 2025 mkoani Morogoro amesema ni muhimu kuzingatia ukusanyaji wa taarifa binafsi unafanywa kwa lengo maalum tu, na kuhakikisha kuwa taarifa hizo hazitumiki nje ya madhumuni yaliyokusudiwa. Kwa kufanya hivyo taasisi hizo zitakuwa zinazingatia misingi ya kisheria ya faragha na heshima kwa haki za watu binafsi.
"Katika dunia ya sasa inayotawaliwa na teknolojia na matumizi makubwa ya taarifa za watu, ni muhimu kwa maafisa wa ulinzi wa taarifa binafsi kuelewa wajibu wao wa kisheria na kiutumishi. Misingi ya ukusanyaji wa idadi ya taarifa kulingana na makusudi husika , usalama wa taarifa, uhifadhi sahihi na usiri ni nguzo kuu katika kulinda haki ya faragha ya mtu binafsi," alisema Bi. HellenΒ
Katika mafunzo hayo, washiriki wamepata fursa ya kujadili mifano halisi ya changamoto wanazokutana nazo kazini na kushiriki katika mazoezi kwa vitendo yaliyowasaidia kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi watakaporudi katika taasisi zao.
Mafunzo haya yanatarajiwa kuwa chachu ya maboresho katika usimamizi wa taarifa binafsi ndani ya taasisi mbalimbali, sambamba na utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini.
ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO
ππππππππ ππππππππ πππ ππππ+ππ ππππβ¦
DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BINβ¦
NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI Wβ¦
DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI Wβ¦
PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFISβ¦
ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIFβ¦
BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODβ¦
JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWAβ¦
NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU Kβ¦
πππππππ ππππ ππ ππππππ ππ ππππππ π β¦
πππππππ ππππππ π ππ πππ ππππ ππππππβ¦
KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YAβ¦
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAGβ¦
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA Bβ¦
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikianβ¦
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUβ¦
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGEβ¦
KARIBU PDPC MHE. ANGELLAH JASMINE β¦
KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUGβ¦