PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFISA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI NCHINI
July 16, 2025, 3:10 p.m.
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ipo katika mpango wa kuwa naΒ Ithibati kwa Maafisa Ulinzi wa Taarifa (DPOs) ili kuhakikisha ulinzi wa taarifa binafsi nchini unazingatiwa.
Hatua hii inalenga kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi na kuhakikisha kuwa waliopewa jukumu la ulinzi wa faragha za taarifa hizo wanazingatia viwango vya juu vya ufanisi na uadilifu.
Hayo yamesemwa leo tarehe 16/07/2025 na Mkurugenzi Mkuu wa PDPC Dkt. Emmanuel Mkilia alipotembelea kituo cha mafunzo maalum ya maafisa ulinzi wa taarifa kilichopo kwenye hoteli ya Morena, Morogoro na kuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo ambapo alisisitiza kuwa mafunzo hayo ni hatua muhimu ya kuleta mazingira rafiki na yenye ufanisi kati ya PDPC na DPOs.
βTunatarajia kuanzisha mfumo wa mafunzo utakaoakisi uthibitisho wa kitaalamu wa DPOs. Hii inamaanisha kwamba, bila cheti rasmi cha utambuzi wako kutoka PDPC, huwezi kuwa DPO halali,β alisisitiza Dkt. Mkilia.
Hii ni hatua madhubuti inayolenga kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi, kuhakikisha maafisa wanaotekeleza majukumu haya wanazingatia viwango vya kitaifa na kimataifa, na kuleta ufanisi wa kiutendaji katika sekta hiyo muhimu kwa ulinzi wa faragha kwenye taarifa binafsi za watu na mashirika nchini.
ROPA NI MUHIMU KWA KILA DPO
ππππππππ ππππππππ πππ ππππ+ππ ππππβ¦
DPO SIMAMIA USALAMA WA TAARIFA BINβ¦
NI LAZIMA KUWA NA SERA YA ULINZI Wβ¦
DPIA NI MUHIMU KUIMARISHA ULINZI Wβ¦
PDPC KUANZISHA ITHIBATI KWA MAAFISβ¦
ELIMU YA DHANA YA ULINZI WA TAARIFβ¦
BALOZI ADADI AONGOZA KIKAO CHA BODβ¦
JENGA UAMINIFU WA TAASISI YAKO KWAβ¦
NI KOSA KUSAMBAZA TAARIFA ZA MTU Kβ¦
πππππππ ππππ ππ ππππππ ππ ππππππ π β¦
πππππππ ππππππ π ππ πππ ππππ ππππππβ¦
KUSAFIRISHA TAARIFA BINAFSI NJE YAβ¦
KAMPENI ZIZINGATIE ULINZI WA FARAGβ¦
ULINZI WA FARAGHA KWENYE TAARIFA Bβ¦
PDPC na NHIF Kuimarisha Ushirikianβ¦
ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUβ¦
DPOs WAIPONGEZA PDPC KWA KUWAJENGEβ¦
KARIBU PDPC MHE. ANGELLAH JASMINE β¦
KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUGβ¦