PDPC YASHIRIKI KIKAO - TATHMINI MRADI WA TANZANIA KIDIJITALI

Feb. 26, 2025, 4:02 p.m. PDPC YASHIRIKI KIKAO - TATHMINI MRADI WA TANZANIA KIDIJITALI

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) inashiriki kikao cha tathmini ya Mradi wa Tanzania ya Kidijitali, kinachofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 24 hadi 27 Februari 2025. Kutoka PDPC kikao hiki kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa PDPC Dkt. Emmanuel Mkilia pamoja na Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji Mhandisi Stephen Wangwe.

Mradi wa Tanzania Kidijitali unatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia na unalenga kuboresha huduma za kidijitali nchini. Maandalizi ya Awamu ya pili ya mradi huu, ambao utaendelea kuanzia mwaka 2026 hadi 2031 yameanza. PDPC itakuwa miongoni mwa taasisi zitakazonufaika kwenye awamu hii, na tunaamini kuwa utachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kidijitali nchini.

Tume inaendelea kujitahidi kuhakikisha kwamba huduma zetu zinakuwa bora zaidi na zinawafaidisha wananachi. Tushirikiane katika kujenga Tanzania ya Kidijitali!