𝐓𝐀𝐁 π–π€πˆπ’π‡π”πŠπ”π‘π” 𝐏𝐃𝐏𝐂 πŠπ”π–π€ππ€π“πˆπ€ π„π‹πˆπŒπ” π˜π€ 𝐃𝐇𝐀𝐍𝐀 π˜π€ π”π‹πˆππ™πˆ 𝐖𝐀 π“π€π€π‘πˆπ…π€ ππˆππ€π…π’πˆ

March 11, 2026, 7:23 p.m. 𝐓𝐀𝐁 π–π€πˆπ’π‡π”πŠπ”π‘π” 𝐏𝐃𝐏𝐂 πŠπ”π–π€ππ€π“πˆπ€ π„π‹πˆπŒπ” π˜π€ 𝐃𝐇𝐀𝐍𝐀 π˜π€ π”π‹πˆππ™πˆ 𝐖𝐀 π“π€π€π‘πˆπ…π€ ππˆππ€π…π’πˆ

Jumuiya ya Watu Wasioona Tanzania (TAB) leo tarehe 11 Machi, 2026 wamepatiwa mafunzo elekezi juu ya dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kuhakikisha kila mtanzania anaielewa vyema Sheria ya ulinzi wa Taarifa Binafsi na kuzingatia utekelezaji wake.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, mwenyekiti wa Jumuiya ya Watu Wasioona Tanzania Bw. Omary Hamisi Itambo, ameishukuru PDPC kwa kukubali kuendesha mafunzo hayo kwa kuwa ni muhimu sana kwa watu wasioona.

β€œTunamshukuru sana Mkurugenzi Mkuu wa PDPC Dkt. Emmanuel Mkilia kwa kukubali ombi letu kuandaa mafunzo haya maalum kwetu. Mmekuja kwa wakati sahihi, tutapata kujua ulinzi wa taarifa binafsi unazingatiwaje hasa kwa watu wenye ulemavu wa kutokuona. Mmetuwezesha kutokuona kwetu kutokuwa sababu ya kuwa nyuma ya mambo ya kitaifa yakiwemo kuzingatia matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi”

Bw. Itambo pia ametumia nafasi hiyo kumuomba Mkurugenzi Mkuu PDPC kulifanya swala hili la kutoa elimu ya dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi hasa kwa watu wasioona kuwa endelevu kwa kuwa waliopatiwa mafunzo haya kwa sasa ni Kundi dogo tu kati ya wengi waliopo nchi nzima.

β€œMkurugenzi Mkuu PDPC Dkt. Mkilia ameenenda sawa na upendo wa Mhe. Raisi kwa kuwa aliagiza wasikilizeni watu wenye ulemavu na kutatua changamoto zao na nyinyi PDPC mmeanza kulitekeleza hili”
β€œKundi unaliloina hapa ni wawakilishi wa watu wasioona. Naiomba Tume yako tukufu ikubali kuendelea kutoa elimu hii ili kujua haki za taarifa binafsi, ulinzi wake ukoje na faida zake ni nini. Ipo mikoa ya pembezoni, ikikupendeza Katavi, Kigoma, Rukwa na Mbeya wapatiwe elimu hii pia. Tunaomba ushirikiano kati ya PDPC na TIB udumishwe kwa kufanya mafunzo haya angalau mara mbili hadi tatu kwa mwaka. Kwa kuwa ulimwengu tunaoishi sasa ni wa kidigiti na kupitia mitandao makosa yanayofanyika ni mengi” amesema Bw. Itambo.

Kwa kuzingatia mahitaji ya watu wasioona, PDPC inatarajia kuiweka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kanuni zake katika maandishi ya nukta nundu