Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amesema kiasi cha Bilion 71.7 za Kitanzania zitatumika kuiunganisha Uganda na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kipindi cha miaka 15. Waziri Nape ameyasema hayo wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Makubaliano ya Kibiashara ya Kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Uganda (NBI) iliyofanyika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 29, 2023. “Leo hii tumeshuhudia utiaji saini wa Mkataba wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano – NICTBB na Mkongo wa Mawasiliano wa Uganda. Mkataba huu una thamani ya kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 28 sawa na fedha za Kitanzania Shilingi Bilion 71.7 kwa kipindi cha miaka 15. Mikongo hii itaunganishwa kupitia mpaka wa Tanzania na Uganda, eneo la Mutukula katika Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.” Amesema Waziri Nape. “Ni matumaini yetu, kuona Afrika ya Kidigital (Africa Digital) inafikiwa na matokeo yake chanya yanasaidia katika kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi na shughuli za kijamii barani Afrika kwa kutumia teknolojia. Ni matumani yetu kuona Afrika yenye mifumo imara ya Serikali Mtandao, Elimu Mtandao, Afya Mtandao, Biashara Mtandao, Kilimo Mtandao katika kutoa huduma kwa wananchi wetu.” Amesema Waziri Nape Aidha, Waziri Nape ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kusimamia vyema kutoa huduma kwa mujibu masharti yaliyopo kwenye mkataba wa makubaliano. “Tuhakikishe tunatoa huduma bora na yenye uhakika, panapotokea changamoto yoyote ile iweze kushughulikiwa kwa haraka. Uganda inategemea huduma bora kutoka kwenu, mkatoe huduma yenye ubora kwa kuzingatia makubaliano ya Waheshimiwa Ma-Rais wetu. Kwa changamoto ambazo zitakuwa nje ya uwezo wenu, mziwasilishe Wizarani kupata ufumbuzi wa haraka”. Amesema Waziri Nape Katika hatua nyingine, Waziri Nape amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania, Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Peter Ulanga na Dkt. Hatwib Mugasa Mkurugenzi Mtendaji wa NITA-U kwa kubeba jambo hili kwa uzito wake na kufanikisha kuungaisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wa Tanzania –NICTBB na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wa Uganda unaosimamiwa na NITA-U. Mkataba huo umetokana mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya kikazi nchini Uganda, ambapo yeye na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoel Kaguta Museveni walikubaliana kuunganisha miundombinu mikuu ya mawasiliano ili kuiwezesha Uganda na nchi jirani kupata huduma za intaneti zenye ubora na bei nafuu na pia kuunganisha nchi ya Uganda na mikongo ya baharini iliyopo Tanzania.
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ) Kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (SJMT) imeandaa Mkutano wa Wadau kuhusu tamko la Amri ya Waziri kuhusu CII na miongozo yake pamoja na mapendekezo ya uridhiwaji wa Mkataba wa Malabo Inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Bima Zanzibar, 29-30 Septemba, 2023. Ndg, Mahfoudh Mohamed Hassan Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi amefungua Mkutano huo Kwa niaba ya Katibu Mkuu WUMU (SMZ), ameeleza kuwa Warsha hii inawaleta pamoja Wadau muhimu sana katika Sekta ya TEHAMa Kwa ajili ya kupata uelewa wa pamoja na baadae kukusanya maoni Kwa upande wa Zanzibar . Aidha, amewaeleza Wajumbe kuwa chimbuko la Miundombinu Muhimu ya TEHAMA na Miongozo yake linatokana na hitaji la kutekeleza Sheria ya Makosa ya Mtandao ( Cybercrimes Act ) ya mwaka 2015 katika Kifungu Cha 28 ambacho kinampa Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana na Mawasiliano uwezo wa Kutambua na Kutangaza Miundombinu muhimu ya TEHEMA (Critical Information Infrastructure - CII) pamoja na miongozo yake. Lengo la kuwepo Kwa Kifungu hiki katika Sheria tajwa ni kuweka nguvu za Kisheria za utambuzi wa Miundombinu muhimu ya TEHAMA Nchini Ili iweze kupewa ulinzi mkubwa na kuhakikisha kuwa huduma za msingi kwa Wananchi zinapatikana. ' Niwaombe sote tushiriki Katika uelimishaji huu kwa makini Ili kuwezesha utoaji wa maoni katika Rasimu ya Tamko la Amri ya Waziri kuhusu Miundombinu muhimu ya TEHAMA na katika mapendekezo ya Uridhiwaji wa Mkataba wa Malabo Ili kuwezesha Wizara zetu kutimiza wajibu katika ujenzi wa Taifa letu' Mkutano huu Umeudhuriwa na Menejimenti ya WUMU, Wakuu wa Taasisi Chini ya WUMU, Viongozi wengine kutoka Taasisi ya WUMU, Wawezeshaji na Watumishi kutoka WHMTH, Watumishi kutoka SMZ, Waandishi wa Habari pamoja na Ndugu Waalikwa.
Tarehe 28 Septemba,2023 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imekutana na Wadau wa Habari kupitia kwa pamoja na kutoa maoni kuhusu rasimu ya sera ya Taifa ya TEHAMA. Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inajukumu la kutunga na kusimamia utekelezaji wa sera ya TEHAMA nchini. Kwa jukumu hilo Wizara iliweza kuanda mkutano huo na Wadau waweze kutoa maoni namna ya sera hiyo itakavyoleta mabadiliko chanya kwa Taifa. Sera hii itaweza kujenga na kulinda usalama wa Wadau na watu wengine katika jamii Kikao hicho kimehudhiriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara pamoja na watumishi wa Wizara na Wadau wa Habari.
Picha Ikionesha zawadi ya T-shirts za Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi alizopewa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP- Bw. Camillius M. Wambura alizopewa na Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Kamshina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bw. Emmanuel L. Mkilia Katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi-Dodoma mnamo 03/05/2024
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Bwana EMMANUEL MKILIA amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Mashtaka, DPP Sylvester Mwakitalu. Katika mazungumzo hayo ambayo yamefanyika leo mei 21, 2024 jijini DODOMA, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuelimisha Tasisi za Umma na Binafsi zinazozochakata taarifa kujisajili kwenye Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi - PDPC kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoagiza mnamo April 03, 2024 wakati akizindua tume ambapo alizitaka Taasisi za Umma kuwa Vinara kwenye kujisajili. Mkilia amesema baadhi ya faida za kujisajili PDPC ni pamoja na wanachi kuziamini taasisi hizo na kuendelea kufanyanazo kazi. Kwa upande wake DPP SYLVESTER MWAKITALU akatumia fursa hiyo kuahidi kutoa ushirikiano wa kikazi na kuboresha mahusiano baina ya taasisi yake na Tume.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Bw. Emmanuel Mkilia leo Jumatano tarehe 5 Juni 2024, amekutana na watumishi wa Tume katika kikao maalumu jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Bw.Emmanuel Mkilia akitoa wasilisho maalum kwenye kikao cha Jukwaa la usalama wa Mtandao Tanzania 2024. Kikao hiki kilipokea ufahamu katika azma ya Tanzania ya kuboresha faragha ya Taarifa Binafsi pamoja na mikakati muhimu inayoendelea kulinda taarifa binafsi katika enzi hizi za kidigitali. #lindataarifabinafsitz #UongoziwaUsalamaMtandao #faraghayakoniwajibuwetu
Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa wa siku mbili wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaohusu ubadilishanaji wa Taarifa Binafsi kwa nchi hizo unaofanyika jijini Kampala (East Africas Data Exchange Forum). Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Bw. Emmanuel Mkilia ametoa taarifa ya hali ilivyo hadi sasa kwa upande wa Tanzania na kuzitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na Mfumo mahususi wa utekelezaji wa matakwa ya makubaliano ya Afrika (Mkataba wa Malabo) na ule wa nchi za Afrika Mashariki. Alisisitiza kuwa utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Tanzania ni kutokana na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia ahadi ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020 ambayo inawahakikishia wananchi kuwa taarifa zao binafsi na faragha zitalindwa ikiwa ni moja pia ya utekelezaji wa Haki za Binadamu kwa watanzania. Aidha Bw. Mkilia pamoja na ujumbe wake wamemtembelea Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli. Hali kadhalika Bw. Mkilia amefanya mazungumzo na wakuu wa Tume za Ulinzi wa Taarifa Binafsi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Bw. Emmanuel Mkilia amekutana na Menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas leo Alhamisi tarehe 13/06/2024 jijini Dodoma. #lindataarifabinafsitz #faraghayakoniwajibuwetu

Kikao kati ya Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bw. Emmanuel L.Mkilia na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Insp.Camillus Wambura katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi MkoanI Dodoma kilichofanyika mnamo tarehe 03/05/2024
Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Bw. Innocent Mungy ameitaka jamii kuchuja taarifa binafsi wanazoziweka mtandaoni ili kujikinga na changamoto za uhalifu wa mtandaoni sambamba na kulinda faragha zao. Bw. Mungy ametoa wito huo jijini Dar es salaam wakati akifanyiwa mahojiano maalum ya kituo cha Redio - TBC Taifa kwenye kipindi cha Asubuhi hii ambapo amesema ulinzi wa taarifa binafsi unaanza na wewe mwenyewe hivyo ni vema kuchuja baadhi ya taarifa binafsi tunazoweka kwenye akaunti zetu za mitandao ya kijamii kwani wapo baadhi ya watu wanauza taarifa hizo na kujiingizia kipato huku wengine wakizidukua na kufanya uhalifu wa kimtandao. Aidha pia Bw.Mungy ametumia fursa hiyo kuzikumbusha Taasisi za Serikali na Binafsi zinazokusanya na kuchakata taarifa kuendelea kujisajili Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoagiza ambapo alisema mpaka kufika Disemba mwaka huu 2024 taasisi hizo ziwe zimeshajisajili ili wateja wao wajihakikishie usalama wa taarifa zao walizoziwasilisha kwao. #lindataarifabinafsitz #faraghayakoniwajibuwetu
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Bw. Emmanuel Mkilia amesisitiza kulindwa kwa faragha za watu hasa kwa kipindi hiki ambacho Tanzania na dunia zinajikita katika Uchumi wa kidigitali. Hayo yameelezwa na Bw. Mkilia kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha TBC kwenye kipindi cha Mizani ikiwa ni moja ya njia ya kutoa elimu kwa umma ili dhana nzima ya Ulinzi wa taarifa binafsi iweze kueleweka kwa jamii wakiwemo wahusika wa taarifa, wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi. “Tumehakikisha Tume ina uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kwa sasa tunatoa elimu kwa umma ili kuleta uelewa wa pamoja kwa mtoa taarifa, wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi, kusimamia sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa kusajili wakusanyaji na wachakataji wa taarifa hizo na kuwapatia vyeti vinavyoonyesha kuwa wapo tayari kufuata sheria hiyo”, amesema Bw. Mkilia. “Kwa sasa hivi kuna huduma nyingi zinatolewa kwa njia ya kidigitali, mteja mkubwa ni huyu muhusika wa taarifa tunayemzungumzia na ili kupata huduma hizo analazimika kutoa taarifa zake binafsi hivyo ni muhimu kujihakikishia kuwa taarifa hizo zinatumika inavyotakiwa na faragha yake inalindwa ili kujenga Tanzania inayojali utu, haki za binadamu na faragha za watu tunavyoendelea kujikita katika Uchumi wa kidigitali”. Pia Bw. Mkilia amezitaka taasisi zote za Serikali na binafsi kujisajili na kuhakikisha wanapata cheti cha usajili cha PDPC ili kujenga imani na kupata fursa ya kutekeleza majukumu yao ndani na nje ya mipaka ya nchi kwa kuwa watakuwa wanazingatia sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi katika utekelezaji wa majukumu yao. Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ni tume huru iliyoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 16 (1) na (2) inayotoa haki ya faragha kwa kila mwananchi na kuelekeza kuundwa kwa chombo cha kusimamia ulinzi wa faragha hizo na ilizinduliwa rasmi tarehe 3 Aprili 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Bw. Emmanuel Mkilia akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Zanzibar (PDPCZNZ), Bi. Rehema Abdallah wamekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware katika ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania leo Ijumaa tarehe 14/06/2024 jijini Dodoma. Viongozi hao wamefanya mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya Taasisi hizo mbili na namna ambavyo TIRA inaweza kuboresha utendaji na utoaji huduma kwa ufanisi zaidi ikiwa na ulinzi madhubuti wa taarifa binafsi. Aidha, Bw. Mkilia yupo ziarani kukutana na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma na Binafsi kuhimiza utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi hususani umuhimu wa kujisajili kwenye mfumo wa PDPC na kuteua Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kila taasisi ili kukidhi matakwa ya Sheria. PDPC inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa Taasisi za Umma na Binafsi kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini waaswa kushirikiana na wafanyakazi wenzao kwenye Taasisi/ Ofisi walizopo ili kutekeleza majukumu yao ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa matokeo chanya. Wito huo umetolewa jijini Arusha na Mwanachama Mwanzilishi wa Chama cha Wataalamu wa Faragha Tanzania - Tanzania (TPPA) Bw. Mrisho Swetu wakati akitoa Mada ya Usafirishaji wa Taarifa Binafsi nje ya Nchi kwenye mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kutoka Taasisi zilizo chini ya chama cha Mabenki Tanzania na chama cha watoa huduma za mitandao ya Simu Tanzania ambapo amesema ni vema Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi akashirikiana na wafanyakazi wenzake kwa ustawi mzuri wa majukumu ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. “Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi unapaswa kuwa na Strategic Engagment na Staff wenzako kwenye Taasisi au Ofisi ili kutekeleza vema majukumu ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwenye Taasisi” alisema Bw. Swetu.
Baadhi ya Picha za matukio ya mafunzo ya Walinzi wa Taarifa Binafsi wa kutoka Taasisi zilizo chini ya Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) na Chama cha watoa Huduma za Mitandao ya Simu Tanzania (TAMNOA), yanayofanyika AICC -Arusha.

Kheri ya siku ya Mashujaa #lindataarifabinafsitz #faraghayakoniwajibuwetu #pdpctz
Majukumu ya Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi
Picha ya ushiriki wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Bw. Emmanuel Mkilia kwenye uzinduzi wa matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM Loliondo tarehe 15 Aprili 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi leo Aprili 03, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. #TaarifaBinafsiTz
Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni miongoni mwa nyenzo muhimu za kufikia uchumi wa Kidigitali Hayo yameelezwa Jijini Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi - PDPC, Bw. Emmanuel Mkilia wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo ya siku nne kwa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kutoka Taasisi zilizo chini ya chama cha mabenki Tanzania - TBA na chama cha watoa huduma za Mitandao ya simu Tanzania - TAMNOA ambapo amesema maendeleo ya haraka ya kidijitali yameonyesha umuhimu mkubwa wa kulinda taarifa binafsi, kuzuia matumizi mabaya ya taarifa na uvujaji wa taarifa binafsi. “Dunia yetu leo inaendeshwa na taarifa mbalimbali, huku taarifa binafsi zikiwa ni njenzo muhimu katika biashara na mwingiliano miongoni mwa watu” Aidha Bw. Mkilia akaweka bayana umuhimu wa Mafunzo haya kwa Maafisa wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini.“Ikizingatiwa Tanzania iko katika jitihada za kuimarisha uchumi wa kidijitali, kundi hili ni muhimu sana katika kuujenga na kuimarisha uchumi wetu kwa kuhakikisha kuwa faragha na taarifa binafsi zinalindwa kwa mujibu wa Sheria yetu ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11 ya mwaka 2022 pamoja na Kanuni zake mbili, kanuni za Usajili na zile za kushughulikia malalamiko ya ukiukwaji wa sheria husika”. Alisema Bw. Mkilia Haya ni mafunzo ya kwanza kwa Maofisa wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi - DPO’s yaliyoandaliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi PDPC kwa kushirikiana na Chama cha Mabenki Tanzania - TBA na Chama cha watoa huduma za Mitandao ya - TAMNOA.
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamisi Abdulla ametoa wito kwa Taasisi na ofisi mbalimbali nchini kuwajengea uwezo maafisa ulinzi wa taarifa Binafsi - DPO’S kwenye kada ya ulinzi wa Taarifa ili kuimarisha sekta hiyo. Bw. Abdulla ametoa wito huo jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya Maafisa ulinzi wa Taarifa binafsi kutoka taasisi zilizo chini ya chama cha mabenki Tanzania - TBA na chama cha Watoa huduma za Mitandao ya simu Tanzania - TAMNOA ambapo amesema hakuna msamaha kwa kutokujua sheria hivyo maaafisa ulinzi wa Taarifa binafsi kwenye Taasisi waelimishwe. “Tume itakua ikiratibu mafunzo haya kwa makundi mbalimbali leo ni kundi la mwanzo na mafunzo ya mwanzo hivyo nitoe Rai kwa Taasisi zote kuhakikisha maafisa wake wanajengewa uelewa na uwezo katika kutekeleza majukum ya Taasisi zao” Aidha Bw. Abdulla akawataka maafisa hao kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia Sera ya Ulinzi wa taarifa Binafsi “ Mabenki na Kampuni za Simu zinafanya kazi katika mazingira yenye ushindani mkubwa na zinahitaji kuwa na Sera na taratibu bora za Ulinzi wa Taarifa binafsi za wateja wao ili kuhakikisha kuwa taarifa za wateja zinakuwa salama na zinalindwa vizuri”. Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi zaidi ya 90 kutoka Taasisi zilizo chini ya chama cha mabenki Tanzania - TBA na chama cha Watoa huduma za Mitandao ya simu Tanzania - TAMNOA wamejitokeza kushiriki mafunzo haya yanayoendeshwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi - PDPC.
WASILIANA NA TUME
TUSHIRIKIANE NA PDPC KUIMARISHA US…
Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi …
TOA TAARIFA ZAKO KULINGANA NA HUDU…
KILA TAASISI IWE NA SERA YA ULINZI…
JAMII X-CHANGE; UBUNIFU KATIKA MIF…